• 7 years ago
Wakati mashabiki wa Simba wakiwa na hamu ya kuona kiungo wao Haruna Niyonzima anarejea uwanjani, mchezaji huyo ambaye yupo nchini India kwa matibabu ametuma salamu.

Niyonzima amesema kuwa afya yake inaendelea vizuri na anashukuru Mungu kwa kuwa anaamini atarejea uwanjani mapema tofauti na alivyotegemea awali.

Mchezaji huyo raia wa Rwanda alikuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa akiuguza jeraha la mguu, sasa amewapa matumaini Wanasimba kuwa anaweza kurejea na kukipiga hata kabla ya msimu hu wa 2017/18 haujamalizika.

Niyonzima amekuwepo India kwa siku kadhaa sasa tangu alipoenda nchini humo wiki jana, anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Jeevika.

Awali ilidaiwa atafanyiwa upasuaji lakini baada ya vipimo hakukuhitajika upasuaji wowote.

Recommended