Ushawishi wa kisiasa kati ya mrengo wa Jubilee na upinzani NASA umesemekana kuanza kushika kasi kabla ya kikao maalum cha bunge Jumanne ijayo na vile vile alhamisi kujadili mapendekezo ya rais Uhuru Kenyatta baada ya kukataa kutia saini mswada wa pendekezo la ufadhili wa fedha za serikali wa mwaka 2018/2019.
Wabunge wanadai kuwa kupendekeza kupunguzwa kwa bajeti za sekta mbali mbali ikiwemo mgao wa fedha za hazina ya maeneo bunge utaibua mihemko ya aina yake.
Category
🗞
News