• 7 years ago
Wimbo Mpya wa Dini | "Jinsi ya Kutafuta Nyayo za Mungu" | God's Sheep Hear the Voice of God

Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu,
lazima tutafute mapenzi ya Mungu,
tutafute maneno ya Mungu na matamshi ya Mungu,
tutafute maneno ya Mungu na matamshi Yake.
Kwani palipo na maneno mapya ya Mungu,
pana sauti ya Mungu, sauti Yake;
palipo na nyayo za Mungu,
pana matendo ya Mungu, matendo ya Mungu.
Palipo na maonyesho ya Mungu,
pana sura, sura ya Mungu,
na palipo na sura ya Mungu,
pana ukweli, njia, na uzima.

Mkitafuta nyayo za Mungu,
mlipuuza maneno kuwa, "Mungu ni ukweli, njia, na uzima."
Hivyo watu wengi wapokeapo ukweli,
hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu
na hata kukosa kutambua kuonekana kwa Mungu.
Ni kosa kubwa sana! Ni kosa kubwa sana!
Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulingana na dhana za mwanadamu,
sembuse Mungu kuonekana kwa ombi la mwanadamu.
Anapofanya kazi Yake, Anafanya chaguo Lake,
Anafanya chaguo Lake, anayo mipango Yake.
Zaidi ya hayo, ana malengo Yake mwenyewe,
na mbinu Zake, mbinu Zake mwenyewe.
Anapofanya kazi Yake, hahitaji kujadili kazi Yake na mtu,
kutafuta ushauri wa mtu, sembuse kumuarifu kila mtu.
Hii ni tabia ya Mungu, inafaa kujulikana na wote.

Ukiwa na hamu kushuhudia kuonekana kwa Mungu,
ukiwa tayari kutafuta nyayo za Mungu,
basi kwanza lazima uvuke dhana zako mwenyewe.
Sharti usimfanyie Mungu madai ya kufanya hili ama lile,
wala hufai kumzuia, katika mipaka yako mwenyewe
na kumwekea mipaka katika dhana zako mwenyewe.
Badala yake, wafaa kuuliza jinsi ya kutafuta nyayo za Mungu,
kukubali kuonekana kwa Mungu,
na jinsi unavyopaswa kutii kazi mpya ya Mungu;
ndilo linapaswa kufanywa na mtu, kufanywa na mwanadamu.
Kwa kuwa hakuna, mwingine aliye ukweli,
na hakuna aliye na, aliye na ukweli,
mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii.
Kwa kuwa hakuna aliye ukweli, hakuna aliye ukweli,
na hakuna aliye na, aliye na ukweli,
mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii.
Mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Injili ya Kushuka kwa Ufalme: https://sw.kingdomsalvation.org/
Kanisa la Mwenyezi Mungu: https://sw.godfootsteps.org/
Kanisa la Mwenyezi Mungu YouTube: https://www.youtube.com/channel/UCkUDnudSY6_KR123N2Yr7mw
Kanisa la Mwenyezi Mungu Facebook: https://www.facebook.com/kingdomsalvationsw/
Kanisa la Mwenyezi Mungu Twitter: https://twitter.com/CAGchurchsw
Kanisa la Mwenyezi Mungu Instagram: https://www.instagram.com/thechurchofalmightygodsw/

Category

🎵
Music

Recommended