• 7 years ago
Swahili Christian Sketch "Onyo Kutoka kwa Historia" (Kichekesho)
Miaka elfu mbili iliyopita, wakati Bwana Yesu alipotokea na kufanya kazi, Mafarisayo walikwamia sheria na kukashifu kazi Yake, wakisema kuwa kazi Yake ilienda zaidi ya Maandiko.Ili kulinda hali zao na maisha yao, walijitahidi kwa nguvu zao zote ili kuwazuia watu kutafuta kazi ya Bwana Yesu, na kujiunga na serikali ya Kirumi kumsulubisha msalabani. Katika siku za mwisho, wakati Bwana Yesu anapoonekana tena katika mwili ili kufanya kazi, viongozi wa ulimwengu wa kidini wanarudia tukio la janga la kihistoria la upinzani wa Mafarisayo kwa Bwana Yesu. Je, wanapingaaje kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Kupitia kwa mchungaji anayeigiza kama Mfarisayo katika tukio, mchezo huu unadhihirisha jinsi wachungaji na wazee wa kisasa wanavyoshikilia Biblia ili kumpinga Mungu, na inaonyesha wazi kwamba njia wanayoitembea ni sawa na ile ya Mafarisayo.

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Maudhui ya video hii yametafsiriwa yote na wafasiri wataalam. Hata hivyo, kutokana na tofauti za lugha n.k., makosa kadhaa yaliyofanywa hayawezi kuepukika. Ukigundua makosa yoyote kama hayo, tafadhali rejea kwa toleo la kwanza la Kichina. Tafadhali jihisi huru kuwasiliana nasi.

Injili ya Kushuka kwa Ufalme: https://sw.kingdomsalvation.org/
Kanisa la Mwenyezi Mungu: https://sw.godfootsteps.org/
Kanisa la Mwenyezi Mungu YouTube: https://www.youtube.com/channel/UCkUDnudSY6_KR123N2Yr7mw
Kanisa la Mwenyezi Mungu Facebook: https://www.facebook.com/kingdomsalvationsw/
Kanisa la Mwenyezi Mungu Twitter: https://twitter.com/CAGchurchsw
Kanisa la Mwenyezi Mungu Instagram: https://www.instagram.com/thechurchofalmightygodsw/
Kanisa la Mwenyezi Mungu Vimeo: https://vimeo.com/thechurchofalmightygodsw
Unakaribishwa kupakua programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu.

Recommended