Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta Jumamosi alimkaripia Mbunge wa Starehe Charles Njagua, maarufu kama Jaguar kuhusu matamshi aliyoyaongea ambayo yanakhisiwa kuleta uhasama baina ya wakenya na watanzania.
Kenyatta alinena haya alipozuru Tanzania kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili. Kenyatta alilakiwa na rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Jaguar alitiwa mbaroni tarehe ishini na sita mwezi wa Juni baada ya kutishia watanzania wote wanao fanya biashara katika masoko ya Gikombaa, Kamkunji na kwengineko ya kwamba watashambuliwa na kisha kufurushwa.
“Wengine wanaongea bila kufikiria, mtu amezoea tu kijiji chake hana uzoefu wa kuzuru maeneo mengine, anafikiria kwamba hapo alipo ndipo mwisho wa dunia, ” Uhuru alifoka.

Category
🗞
News