• 7 years ago
Idadi ya watu walioangamia nchini Tanzania kwenye mkasa wa ferry kuzama katika ziwa Victoria imefikia watu 126.
Ferry hiyo ya John Magufuli ilizama Alhamisi jioni ilipokuwa ikitoka  kisiwa cha Bugorora kuelekea kisiwa cha ukara ikiwa imebeba takriban abiria 300, wengi wao wakiwa wafanyibiashara.
Rais Uhuru Kenyatta ameelezea kusikitishwa kwake na mkasa huo na kumpa pole rais John Magufuli na raia wa Tanzania kwa niaba ya wakenya.

Category

🗞
News

Recommended