• 7 years ago
Maaskofu Wa Kanisa la Roman Catholiki, Wametoa Ujumbe wa Kwaresma wa Kulaani hali mbaya ya Udictator, Mauaji na Uonevu Nchini Tanzania, Na pia wakatoa Mwito wa Kuwepo Kwa Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi. Kiongozi mwenzao Cardinal Policarp Pengo alisaliti sauti yao ya Haki na Akadai Wamechanganya Dini na Siasa. Ni Kwa Usaliti Huo Nasema Pengo Alaaniwe na Kila Mtanzania Mpenda Haki.

Kadhalika Maaskofu 27 Wa Kanisa la Kilutheri Tanzania KKKT wakiongozwa na Akofu Mkuu, Askofu Shoo, Wametoa Waraka wenye Maudhui Unaofanana Na Huo, Tofauti Ni Kuwa Askofu Kiongozi Wao, Mwenye Kumjua na Kumhofu Mungu, Mwenye Kujali haki Amesimama Pamoja na Maaskofu Wenzake, Ndio Sababu Nasema Tuwatakie Baraka na Amani Maaskofu hawa. Akiwemo Askofu Mkuu Shoo.

Kadhalika Pamoja na Kuwa Sijawahi Kupata Fursa ya Kusema au Kukutana na Mwenyekiti wa Chadema Mbowe! Napenda Kumwenzi kama Kiongozi Mzalendo, Kiongozi Muungwana, Kiongozi Mwenye Utu, Na Kiongozi Mwenye Busara Mara 1000 Kuliko Magufuli. Kukamatwa Kwake kwa Kesi za Kubambikiwa na Kupakiwa Kwenye Kilori (Pickup) Ni Udhalilishaji, Ni Kitendo cha Kuhuzunisha sana! Ni Tanzania Tu Upuuzi wa Namna Hii Unaweza Kufanyiwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani, Mwenye Wabunge zaidi ya 100 Bungeni. MAGUFULI FREE, FREEMAN MBOWE UNCONDITIONALY NOW!

Recommended